Image
person holding up a mobile phone, taking a photo

Photo: Albin Hillert/WCC

Baada ya timu ya mawasiliano ya WCC kutengeneza miongozo hii baada ya warsha za ndani, Sy-ovata Shalon Kilonzo, afisa mawasiliano wa WCC aliyepo Nairobi, Kenya, alishiriki utaalamu wake kulingana na uzoefu wake katika Mtandao wa Kiekumeni wa Watetezi wa Walemavu wa WCC. Hapa chini, Kilonzo anashiriki tafakuri kadhaa kuhusu umuhimu wa mawasiliano jumuishi na yanayofikika. 

Nani atakayetumia miongozo hii?

Kilonzo: Ninatumaini miongozo hii itatumiwa na wafanyakazi wote wanaohusika katika idara ya mawasiliano ya WCC na kuwahamasisha wengine kufuata. Ninaamini watachangia kuhakikisha kwamba mawasiliano yanayotoka WCC yanadumisha ujumuishi na ufikiaji.

Nini kilichokupa wasiwasi zaidi wakati wa janga la COVID-19? 

Kilonzo: Kama mtu wa mawasiliano, nina wasiwasi kuhusu kutokuwepo ufikiaji wa taarifa kuhusu COVID-19 kwa ujumla na kwa umahususi chanjo ya COVID-19. WCC imekuwa ikizalisha zana nyingi sana ambazo husadia kondoa tatizo hili, na kusaidia kuwapa watu si tu taarifa sahihi bali pia hisia ya tumaini na hamasa kwa ajili ya siku zijazo.

 

Kwa mtazamo wako, kwa nini maneno tunayoyachagua ni muhimu sana?

Kilonzo: Maneno yanabadilisha ulimwengu. Maneno yanaweza kutofautiana sana kimaana kwa makundi tofuati ya watu. Kwa maneno yako, unaweza kuchangia bila kujua mtu kuhisi kuwa ni mtu wa nje. Uchaguzi wa maneno katika mawasiliano yetu ni muhimu sana tunaporejelea watu wenye ulemavu. Kutumia maneno sahihi katika mawasiliano yetu ni njia moja wapo ya kuchangia katika kutambua msimamo imara wa WCC ambao ni jumuishi zaidi kwa ajili ya haki za binadamu za watu wote.

Je, unaweza kushiriki orodha-kaguzi ndogo ya baadhi ya vidokezi vya mawasiliano jumuishi? 

Kilonzo: Ninafurahi kufanya hivyo! 

Tovuti

Jumuisha maandishi kama mbadala wa picha; maelezo ya data iliyowasilishwa kwenye chati, michoro, na vielelezo; lebo kwa ajili ya udhibiti wa fomu, maoni na vipengele vingine vya kiolesura cha mtumiaji. 

Wezesha/amilisha ubadilishaji wa ukubwa wa maandishi kulingana na upendeleo wa mtumiaji kwenye tovuti. 

Kuhakikisha utofautiano wa rangi kati ya mwonekano wa mbele na wa nyuma ni imara vya kutosha. 

Bado inachukuliwa kuwa ni desturi nzuri kutochapisha kitu chochote kidogo kuliko ukubwa wa maandishi aina ya Arial 12. 

Vipengele vya habari

Usitaje ulemavu wa mtu isipokuwa kama ni lazima kwenye kisa chochote.

Tumia lugha ya watu kwanza (watu wenye ulemavu), ambayo ndiyo lugha inayotumika kwenye Mkataba wa Haki za Binadamu za Watu wenye Ulemavu. Kuna vighiri kadhaa. Kwa mfano, tunaporejelea watu ambao ni vipofu, tunaweza kusema ama "vipofu" au "watu wenye upofu".

Mitandao ya kijamii

Tumia maandishi mbadala kadiri iwezekanavyo, hasa pale ambapo picha inajumuisha taarifa ambazo zinaelezea zaidi ujumbe wa maandishi wa chapisho hilo.

Epuka vifupisho ambavyo vinaweza kuwa vigumu kutafsiri.

Video

Kwa mafaili ya video yanayoonyeshwa mtandaoni ambayo hayana maelezo, toa maandishi katika mfumo wa faili la Word au PDF, au angalau useme kwamba maandishi yanapatikana ikiwa itaombwa hivyo. Fikiria kuweka ishara za kimataifa (Shirikisho la Kiulimwengu la Viziwi) kwa ajili ya viziwi na watu wasiosikia vizuri.

Kiunganishi cha kupata miongozo ya mawasiliano

Kiunganishi cha EDAN