Displaying 1 - 1 of 1

Mawasiliano jumuishi: "maneno yanabadilisha ulimwengu"

Idara ya Mawasiliano ya Baraza la Makanisa la Kiulimwengu (WCC) imechapisha miongozo mipya ya ndani ili kuhakikisha yanakuwapo mawasiliano jumuishi na yanayofikika. Hivi karibuni, idara ya mawasiliano ya WCC imekuwa ikifanya jitihada za kuwa na mawasiliano ambayo ni jumuishi zaidi na yanayofikika. Mfano mmoja wapo ni ule ambapo utengenezaji wa tovuti mpya ya WCC ulizingatia mahitaji ya ufikiaji kwa watu wenye ulemavu. Mfano mwingine: WCC imekuwa ikifanya majaribio ya ukalimani wa lugha ya ishara kwenye mikutano ya mitandaoni. Mwaka 2021, timu ya mawasiliano ilichunguza njia zaidi za kuhakikisha kazi ya mawasiliano yetu inakuwa jumuishi na inadumisha ufikiaji wa hali ya juu tunapojiandaa kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 11 wa WCC utakaofanyika Karlsruhe—na zaidi. Yote haya yalilazimisha kuwepo na uhitaji wa kuwa na miongozo kwa ajili ya mawasiliano jumuishi na yanayofikika.