Displaying 1 - 1 of 1

Kusitasita kukubali chanjo kunaleta tena changamoto nyingine

Wakati mipango ya utoaji chanjo ikifanyika katika nchi zaidi na zaidi, kuna matumaini ya kumalizika kwa janga ambalo limeleta hofu na wasiwasi kote ulimwenguni tangu mapema mwaka 2020. Kurudi katika hali ya kawaida ya maisha ya kila siku, ambapo watu wanaweza kushirikiana na familia na marafiki, kwenda kazini kama walivyokuwa wakifanya na kumwabudu Mungu pamoja kanisani siku za Jumapili, kunasubiriwa kwa hamu.